Wapendwa, jana ndiyo siku tuliyompumzisha ndugu yetu Che Chigwele Salum Josephat Mohamed Mundugwao aliyezikwa juzi, katika makaburi ya Tegeta kwa Ndevu mnamo majira ya saa 10 Alasiri. Picha kama zinavyojieleza tangu tukiwa nyumbani kwenye dua, kisha makaburini na taswira yake mwenyewe enzi za uhai wake. Tumempoteza mwanamuziki mahiri wa miondoko ya muziki wa asili pia rafiki mwema na mcheshi, ambaye hakujenga matabaka ya aina yoyote katika maisha yake.
Hilo lilidhihirika jana katika msiba kwa makundi mbalimbali tofauti yaliyohudhuria maziko, inna lilahi wainna ilahyi raajiun! Ni hayo tu kwa sasa wapendwa.
Wakatabahu.
Habari na picha kwa hisani ya msanii +Innocent Nganyagwa




No comments:
Post a Comment