Friday, 4 October 2013

PRODUCER MAN WALTER & MSANII 20% WAPATANA.

KATIKA HALI ILIYOPONGEZWA NA WAPENZI WENGI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NCHINI,NI KITENDO CHA MSANII 20% NA PRODUCER WAKE WA AWALI MAN WALTER KUWEKA TOFAUTI ZAO PEMBENI NA KUPATANA KURUDISHA HESHIMA YA SANAA YA MUZIKI ILIYOONEKANA KUTAKA KUPOTEA KWA MSHINDI HUYO WA TUZO TANO MFULULIZO{20%}KUPITIA KILI MUSIC AWARDS, KIHISTORIA HII HAIFICHIKI KABISA KWANI PRODUCER MAN WALTER NDIYE ALIYEFANIKISHA MAFANIKIO MAKUBWA YA MSANII 20%,IKIWEMO KUTWAA TUZO HIZO TANO MFULULIZO KUPITIA ALBAM YAKE ILIYOVUNJA REKODI"FURAHA IKO WAPI"
KATIKA KULIWEKA BAYANA HILO PRODUCER MAN WALTER,AMEFUNGUKA KUWA WAMEPATANA NA MSANII 20% NA KUAMUA KUWEKA TOFAUTI ZAO PEMBENI,AKISISITIZA HILO MAN WALTER,AMEDAI KUWA KWA SASA WAPENZI WA BONGO FLEVA NA WAPENZI WA 20% WAKAE TAYARI KUMPOKEA 20% AKIJA NA STYLE NYINGINE KABISA KUTOKA MIKONO YAKE{MAN WALTER},AKIDAI KWA KUPOTEA KWA 20%,WASANII WENGI WAMEJARIBU KUFANYA STYLE KAMA YA 20% LAKINI WAMESHINDWA KUIFANYA KAMA ALIVYOIFANYA YEYE AWALI,IKIWEMO MA PRODUCER PIA,KITENDO KINACHOMSUKUMA YEYE{MAN WALTER}KUTAMBULISHA STYLE NYINGINE KUPITIA MSANII 20%,STYLE ALIYODAI ITABAMBA ZAIDI YA ILE YA AWALI..

No comments: