Thursday, 13 February 2014

MBIO ZA URAIS 2014,WATATU WAHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI{CCM}

Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Phillip Mangula  JANA iliwahoji watu watatu ambao wawili walishawahi kuwa Mawaziri Wakuu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Mawaziri hao waliohojiwa leno ni Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa,Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye na Mbunge wa Sengerema Ndugu William Ngeleja ambaye pia alishawahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Kamati hiyo bado ina kazi ya kuwahoji viongozi wengine watatu ambao leo walishindwa kufika baada ya kuomba hudhuru kwani walikuwa na majukumu mengine ya kiserikali, ambao hawajafika leo ni Waziri wa Mambo ya Nje Ndugu Bernard Membe ambaye yupo safarini nje ya nchi ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Ndugu Stephen Wassirana Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Ndugu Januari Makamba
Mahojiano haya yanalenga moja kwa moja harakati zinazoendelea kwenye UCHAGUZI mkuu ujao kwa mwaka 2015,na hii ni kwa mujibu wa taharifa za ndani kuwa viongozi waliohitajika na kamati hii ya maadili kwa mahojiano ni wale walioonyesha nia na kuzianza kampeni chini chini kuelekea uchaguzi wa RAIS,WABUNGE na MADIWANI kwa mwaka 2015,wakati muda sahihi wa kampeni haujawadia.. 
Mawaziri wakuu wastaafu,Bw,FEDRICK SUMAYE na Bw EDWARD LOWASA wakiw ndani ya jengo la makao makuu{CCM}tayari kwa kuhojiwa.
  
Mh,Waziri mkuu mstaafu Bw,FEDRICK SUMAYE akiwasili kwenye makao makuu{CCM}Dodoma tayari kwa kuhojiwa na kamati ya maadili{CCM}
wanahabari wakijaribu kupata habari kuhusiana na kilichokuwa kikiendelea kwenye mahojiano hayo,
 

No comments: