Habari kutoka Somalia zinasema kuwa mshambuliaji wa kujitoa muhanga amejilipua ndani ya gari na kuwauwa watu 12 na kujeruhi wengine wanane.
Mlipuko huo umetokea nje ya makao makuu ya maafisa wa usalama .
Mwandishi wa BBC anasema kuwa waliofariki ni maafisa usalama na wengine raia wa kawaida waliokuwa katika mgahawa uliopo karibu na jengo hilo.
Kumekuwa na ongezeko la mashambulizi nchini Somalia huku vikosi vya nchi hiyo vikipambana na wanamgambo wa al shaabab wanaofanya matukio tofauti tofauti.
SOURCE:-BBC SWAHILI.
No comments:
Post a Comment