Saturday, 8 February 2014

MOVIE MPYA YA Dr CHENI INAYOONGELEA USHOGA YAZUIWA NA BODI YA FILAMU{TZ}-TFB

SIKU chache baada ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kuzuia filamu ya mkongwe katika sinema za Kibongo, Mahsein Awadh Said ‘Dk. Cheni’ ijulikanayo kwa jina la NIMEKUBALI KUOLEWA isiingie sokoni kwa madai kuwa imekiuka maadili ya Kitanzania,

Dr,CHENI anadai kusikitishwa sana na maamuzi ya bodi hiyo huku akidai kuwa lengo la filamu hiyo ni kukemea tabia za kishoga zinazoendelea kuibuka kwa vijana ikiwa ni pamoja na kupinga uhalali wa ndoa za jinsia moja.Katika maelezo hayo, DK. Cheni ambaye huzitendea haki vilivyo filamu zake kwa kuvaa uhusika halisi, alisema moja ya kigezo ambacho bodi hiyo imekitumia kuzuia filamu hiyo ni pamoja na muonekano wa bango la filamu hiyo ambalo linamuonyesha msanii huyo akiwa amevaa vazi la shela huku akiwa amejiremba kwa madai kuwa ni kuchochea ushoga jambo ambalo msanii huyo amelipinga vikali.
 “Eti ushoga wangu uko kwenye kujiremba sana, hakika wamenionea sana, lengo letu ni kuonya na kukemea vikali vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja, huwezi kuelimisha bila kuonyesha madhara yake kwa vitendo kama ilivyo ndani ya filamu hiyo.Alisisitiza Cheni.
 Ndani ya filamu hiyo ya Dr,Cheni kuna kipande ambacho kinaonyesha kiongozi wa serikali akikemea kitendo hicho, sasa hapo ushoga wangu uko wapi? Kuvalia shela kwenye kava? Siyo sahihi kabisa,” alisema Dr. Cheni.

Mbali na kava hilo, msanii huyo alidai haoni kosa lolote katika filamu hiyo hivyo ataendelea kupigania haki yake na kwamba hayuko tayari kuonewa.
 Jitihada za kumpata mkurugenzi wa bodi ya filamu nchini,Bi, Joyce Fissoo ili kuelezea juu ya sekeseke hilo, ziligonga mwamba,huku taharifa za ndani toka ndani ya Bodi hiyo zikidai kuwa Bodi hiyo itaendelea kusimamia msimamo wake huo huo wa kuizuia filamu hiyo Isiingie Sokoni.
Source:-GLOBAL PUBLISHER{GPL}

No comments: