Saturday, 8 February 2014

MSANII ELIZABETH MICHAEL KUSOMEWA SHITAKA LAKE LA KUUA BILA KUKUSUDIA SIKU TATU BAADA YA VALENTINE DAY.

ELIZABETH MICHAEL"LULU"
Supastaa wa filamu za Bongo{Bongo Movie}, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ atapandishwa  kizimbani kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania kwa tuhuma ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa nyota wa movie nchini, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’,
Lulu atasomewa Shitaka lake Februari 17, mwaka huu na Jaji Wa Mahakama Kuu Rose Temba,hii ni siku tatu baada ya kilele cha maazimisho ya sikukuu ya wapendanao "Valentine Day"“Elizabeth Michael(Lulu) atasomewa upya mashitaka ya kumuua Hayati Steven Kanumba bila kukusudia,hii ni kutokana na marekebisho ya kesi hiyo kufanywa upya na Mahakama Kuu,kutoka Shitaka la mwanzo la kuua kwa kukusudia na kuwa la Kuua bila kukusudia.
Kwa mujibu wa taratibu za Kimahakama“Lulu"Atatakiwa kuulizwa maswali mawili tu,kama ni kweli ameua au si kweli? Naye atatakiwa kujibu swali moja kati ya hayo mawili, kama ni kweli atasema kweli na kama si kweli atasema si kweli,” 

Taharifa zinasisitiza kuwa kesi hiyo itaendeshwa kwa siku mia saba na thelathini (730), kwa maana ya miaka miwili hadi hukumu itakapotolewa,hii ni kwa mujibu wa sheria mpya kwa kesi zote za jinai nchini.
Katika Siku ya Sheria Duniani iliyoadhimishwa jijini Dar es Salaam, Februari 3, mwaka huu, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman alisema kuanzia sasa kesi zote za jinai zitatakiwa kumalizika katika kipindi cha miaka miwili.
Kesi ya Lulu nayo ni ya jinai na kwa sababu hiyo, hadi Februari ya mwaka 2016 itatakiwa iwe imemalizika.

WAKILI WA LULU Bw,PETER KIBATALA.
Pia kwenye kesi hiyo Lulu atatetewa na yuleyule wakili wake mwenye ‘ngekewa’ ya kuwatetea watu maarufu nchini, Peter Kibatala.
Kibatala ameshawahi kuwa wakili wa Mbongo Fleva, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ katika kesi ya madai ya kuiba ‘power window’ ya gari la msanii mwingine wa Bongo Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
Pia aliwahi kumwakilisha wakili mwezake, Mabere Nyaucho Marando kwenye kesi ya Mbongo Fleva, Judith Wambura ‘Anaconda’ alipoburuzwa kortini na uongozi wa Clouds Media Group baada ya Marando kuwa na udhuru.
Pia Wakili Kibatala ilibaki kidogo awe wakili wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu katika kesi ya kumpiga makofi meneja wa hoteli moja (jina tunalo) iliyopo Kawe Beach, Godluck Kuyumbu lakini akakosa sifa baada ya shauri hilo kusiklizwa Mahakama ya Mwanzo Kawe, Dar.
kuna watu muhimu ambao mahakamani itawahitaji ili kutoa msaada wa kufanikisha upatikanaji haki juu ya kesi hii yenye mvuto mkubwa kwa jamii ya Watanzania,
1-Mmoja kati ya wanaosadikiwa kuhitajika na mahakama kwa ajili ya ushahidi ni pamoja na  Aliyekuwa akimtibu Kanumba, Dokta Kidume yeye anaweza kuhitajika kufika mahakamani hapo kwa sababu ndiye aliyekuwa mtu wa pili  kufika kwenye chumba cha marehemu mara baada ya kuanguka.
SETH BOSCO{MDOGO WAKE MAREHEMU}

2-SETH BOSCO
Huyu ni ‘mdogo’ wa marehemu Kanumba, yeye siku ya tukio alikuwa nyumba moja na marehemu, ila vyumba tofauti. Ndiye aliyemwona Kanumba akiwa katika hali mbaya baada ya kutoelewana na Lulu na kukimbia kumwita Dokta Kidume.  

Hawa wote walishahojiwa na Jeshi la Polisi Tanzania katika Kituo cha Oysterbay, Dar, mara baada ya kifo hicho. Seth alihojiwa mara tano.
HAYATI STEVEN KANUMBA"THE GREAT"
 Hayati Steven Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam. Huku Kifo chake kikidaiwa kutokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa na hivyo kuufanya ubongo kutikisika (brain concussion). Hata hivyo, baadaye ilifahamika kuwa, sehemu ya maini na majimaji ya machoni vilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kulikuwa na sumu au kitu kingine katika mwili wa Kanumba. ambapo Majibu juu ya Uchunguzi huo hayajatoka hadi leo.
Wakili anayemtetea msanii Elizabeth Michael alikataa kuongea lolote alipofuatwa na wanahabari kwa ajili ya kulitolea ufafanuzi suala hilo la shitaka jipya kwa mteja wake huku akidai yuko bize na shughuli zake za Uwakili,akiahidi kuonana nao Mahakamani.

No comments: