Kwa mujibu wa baadhi ya waumini hao, ilifika mahali mtumishi huyo wa Mungu alishindwa kuendelea na mahubiri, ikabidi atolewe na huduma yake kuchukuliwa na wasaidizi wake.
“Baada ya kutolewa madhabahuni tuliamini hali itapoa baada ya kupumzika kidogo, lakini wapi? Hali yake ilizidi kuwa mbaya, sasa alikuwa hawezi kuzungumza sawasawa,” alisema muumini mmoja wa kanisa hilo.
Habari zaidi zinasema kuwa, ilipoonekana mtumishi huyo hapati nafuu, mkewe, Anna Suguye kwa ushirikiano na waumini wengine walichukua gari na kumkimbiza Hospitali ya African Medical Investment (AMI) iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam ambako alilazwa kwa matibabu ya awali. Ikumbukwe kuwa hata Askofu Moses Kulola alifia kwenye hospitali hiyohiyo pia.
Wakati mchungaji huyo anapelekwa hospitalini, baadhi ya waumini walikuwa wakibubujikwa machozi kwa vile walikuwa hawajui hatima ya kiongozi wao huyo.
“Kwanza namshukuru Mungu wangu amenipigania hadi leo hii naongea nanyi. Kwa mujibu wa daktari nililishwa sumu kali sana japokuwa Daktari hakuniambia ni Sumu ya aina gani. Ila aliniahidi majibu kamili nitayapata baadaye leo.”alisema Nabii Suguye.....“Nakumbuka ilikuwa Januari 28, mwaka huu ndipo nilianza kupata maumivu makali. Nilikuwa nikiendelea na ibada kanisani wiki nzima huku nikipata maumivu.
“Hata hivyo, nilikuwa nasali bila kujua ni kitu gani kilikuwa kikinisumbua kwenye mwili wangu. Nilifikiri ni ugonjwa wa kawaida ambao ningeweza kupata nafuu haraka lakini haikuwa hivyo.
Nabii Suguye aliendelea kusema kuwa kikubwa kilichokuwa kikimsumbua kwa wakati huo ni kutapika huku mwili ukifa ganzi ndipo siku ya ibada akazidiwa na kukimbizwa hospitali.
“Pia daktari aligundua presha yangu ilishuka sana, nilitundikiwa dripu ya maji na kuchomwa sindano ya kupunguza maumivu.
“Hata hivyo haikusaidia, ikabidi wanichome sindano nyingine na kuchukua vipimo vya damu na picha ya X-ray, japo hawakubaini kitu pia. Halafu pia nikawa sipati choo, nikijisaidia inatoka damu.
“Vipimo walivyochukua baadaye walibaini sumu niliyolishwa ilikuwa ya muda mrefu, tena ni Mungu bado ananipenda kwani sumu hiyo daktari alisema ni kali na nisingeweza kuchukua muda mrefu nikiwa hai,” alisema Suguye.Akizungumzia hisia zake juu ya nani yuko nyuma ya sumu hiyo, Nabii Suguye alisema:
“Huenda wakawa wapinzani wangu wa huduma ya Mungu lakini kumjua ni nani, ilikuwa wapi na lini nilipewa si rahisi.”
Baadhi ya watu wenye majina makubwa waliowahi kulishwa sumu na kunusurika kifo ni pamoja na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (hakutaja hospitali), msanii wa filamu za Bongo, Illuminata Poshi ‘Dotnata’ (alikimbizwa Lugalo) na aliyewahi kuwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, SACP Charles Kenyela (alikimbizwa TMJ). Wote hawakukumbuka siku ya kukutwa na tukio.
No comments:
Post a Comment