WASANII mbalimbali katika nyanja za sanaa leo wameungana katika
ukumbi wa Vijana, Kinondoni katika kuzindua rasmi kampeni ya
kuhakikisha mapendekezo yao kikatiba yanasikilizwa na kupitishwa.
Akizindua kampeni hizo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Lebejo Mngereza alisema:
“Tupo pamoja na wasanii wote, tutahakikisha wasanii wetu wanasikilizwa na kutekelezewa maombi yao kwenye katiba mpya. Haiwezekani msanii kukosa haki zake za msingi kwa muda mrefu.” Alisema.
Awali, Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) wakishirikiana na Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TAMUNET) waliandaa na kupeleka mapendekezo mawili yaliofikishwa kwenye Tume ya Katiba.
Pamoja na kupokelewa hapakuwepo na jambo lolote lililotokana na mawazo hayo ambalo lilichukuliwa na kuingizwa kwenye Rasimu ya Katiba.
Mapendekezo mawili waliokuwa wameyatoa awali ni pamoja na kutaka wasanii kutambuliwa katika Katiba kama moja ya makundi maalum, kama vile walivyotajwa wavuvi, wakulima, wafugaji na kadhalika.
Pendekezo la pili lilikuwa ni kuweka kipengele cha kulinda na kuendeleza Haki Miliki na ubunifu katika Katiba mpya.

No comments:
Post a Comment