Wednesday, 5 February 2014

WATU MAARUFU WANAOSHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA LEO.

WATU WENGI MAARUFU WAMEGONGANISHA SIKU ZA ZA KUZALIWA LEO,NA KUSABABISHA SIKU YA LEO KUBEBA KUMBUKUMBU KUBWA KWA WATU HAWA MAARUFU DUNIANI
CRISTIANO RONALDO:-
Mwanasoka tegemeo wa Timu ya Real Madrid na Timu yake ya Taifa ya Ureno,ambaye mwaka  huu mwezi January ametangazwa Rasmi kuwa ndiye mchezaji bora kwa mwaka 2013{FIFA BALLON D'OR 2013}
NEYMAR:-
Mchezaji soka toka klabu bora nchini SPAIN{FC,BARCELONA}na Timu ya taifa ya BRAZIL,pia naye leo ni siku yake ya kuzaliwa.

ADNAN JANUZAJ:- 
Straika mkali na mwenye umri mdogo toka timu maarufu nchini UINGEREZA "MANCHESTER UNITED" ADNAN JANUZAJ naye leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa pia.
CARLOS TEVEZ:-
Straika mkali na mwenye nguvu nyingi za miguu zinazomuwezesha kupiga mabao kwa uwakika CARLOS TEVEZ{ARGENTINA}naye leo ni mmoja kati ya watu maarufu wanaosherehekea siku ya kuzaliwa.
 TOYA DELAZY:-
Ni Mwanamuziki kipenzi cha Vijana wengi wa jinsia zote nchini AFRICA YA KUSINI na AFRICA kwa ujumla TOYA DELAZY,ni mzaliwa na mkazi wa AFRICA YA KUSINI,pia naye leo ni siku yake ya kuzaliwa.
BOBBY BROWN:-
Robert Barisford"Bobby Brown"mwanamuziki mkongwe wa muziki wa RnB,Mwandishi mzuri wa Nyimbo,Rapper na Dancer aliyetokea kwenye kundi lililozalisha vipaji vingi maarufu katika muziki wa RnB duniani"THE NEW EDITION"naye ni mmoja kati ya wanaosherehekea siku ya kuzaliwa leo.
CAM'RON:-
Camron ni msanii mkongwe katika muziki wa Hip hop duniani jina lake ni moja kati ya majina makubwa yenye historia kwenye muziki wa hip hop duniani,CAMRON anawakilisha LEBO ya DEF JAM Kimuziki ,leo hii naye pia anasherehekea siku yake ya kuzaliwa{Birthday}






No comments: