Kumekuwa na
kurasa (accounts) mbalimbali zenye jina la Mh. Edward Lowassa Waziri
Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mitandao ya
kijamii Kama vile Facebook,Twitter,Instagram nk.
Zinazoonyesha kuwa mmiliki wake ni Mh. Edward Lowassa.
Ukweli ni kwamba hizo kurasa zote hazimilikiwi na Mh. Lowassa.
Kwa maana hiyo chochote kinachoandikwa au kuchapishwa kwenye kurasa hizo,hakihusiani kwa namna yoyote na Mh. Lowassa.
Hata hivyo Mh.
Lowassa anawashukuru wote wenye kumiliki account hizo bila ya ruhusa
yake, kwani anaamini wamesukumwa na mapenzi yao kwake.
![]() |
| PICHANI WAZIRI MKUU Bw,MIZENGO PINDA AKIONGEA JAMBO NA WAZIRI MKUU MSTAAFU Mh,EDWARD LOWASA BUNGENI DODOMA. |


No comments:
Post a Comment