Maafisa wa utawala katika jimbo la Washington nchini
Marekani, wamepata miili sita zaidi hii ni baada ya maporomoko ya ardhi
yaliyotokea siku ya Jumamosi.
Maporomoko hayo yamefikisha idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko hayo kufikia 14.mpaka sasa Watu 176 bado hawajapatikana baada ya ukuta wa matope wenye urefu wa futi 177 kuporomoka karibu na mji wa Oso, Kaskazini mwa Seattle.
Waokozi wangali wanaendelea na shughuli ya kuwatafuta manusura kwa kutumia helikopta na miale ya Laser.
Lakini maafisa wanakiri kuwa wana matumaini madogo sana ya kupata manusura.
Rais Barack Obama ametangaza hali ya hatari katika jimbo hilo na kuwaamuru maafisa wote wa serikali ya jimbo hilo kushirikiana kutoa msaada wa dharura.
Gavana wa jimbo hilo ameitaja hali kuwa mbaya na ambayo haikutarajiwa.
Watu 176 bado hawajapatikana.
Jamaa na marafiki pamoja na wafanyakazi wa kujitolea, wanatumia misumeno na mikono mitupu kuondoa vifusi ili kutafuta wale waliopotea.
No comments:
Post a Comment