![]() |
Putin na Obama |
Rais wa Urusi Vladmir Putin ametia saini ilani ya
katiba inayotambua jimbo la Crimea kama taifa huru. Hatua hiyo inajiri
muda mfupi baada ya marekani na Muungano wa Ulaya kutangaza vikwazo
dhidi ya maafisa wa serikali ya Urusi na wa Ukraine waliohusika na njama
ya Moscow kuiondoa Crimea katika Ukraine.
Rais Obama amesema kuwa anataka kuweka bayana
kwamba kutakuwa na adhabu kwa wale walioanzisha mikakati ya Crimea
kujitenga na Ukraine akiongeza kuwa vikwazo zaidi vitatolewa. Hata hivyo
amesisitiza kuwa bado kuna njia ya kusuluhisha mzozo huo kwa njia ya
kidiplomasia.Awali bunge la Crimea lilitangaza rasmi kuwa jimbo hilo liko huru kutoka kwa Ukraine na kutoa maombi ya kujiunga na mataifa yanayobuni muungano wa Urusi. Balozi wa Marekani nchini Ukraine, Geoffrey Pyatt, ameiambia BBC kwamba ilani iliyotiwa saini na rais Putin kutambua uhuru wa Crimea haitabadili mtizamo wa Marekani kuhusu hali ilivyo.
" Kadri marekani inavyozingatia, hapatakuwa na mabadiliko kuhusiana na makadirio yetu kuhusu hali, mtizamo wetu wa Crimea kama sehemu ya Ukraine iliyo huru na mtizamo wetu kuhusu kwamba kura ya maamuzi ya siku ya jumapili iliyofanyika baada ya uvamizi wa kijeshi uliotekelezwa na Urusi ni kinyume na sheria kwa vyovyote," anasema.
![]() |
Mwanajeshi wa Ukraine karibu na jimbo la Crimea. |
"Uwezo wa kutoa vikwazo dhidi ya watu mbali mbali upo. Tutatoa tathmini kuhusu hatua muafaka wakati hali ikiendelea kubadilika. Hatutawasaza baadhi ya watu. Kutakuwa na gharama kwa Urusi, Gharama ya ziada itakayotolewa kwa Urusi, ikiwa Urusi haitabadili mwelekeo wake kuhusiana na jinsi inavyoshughulikia hali nchini Ukraine," anasema.
Miongoni mwa maafisa waliolengwa na vikwazo vya Marekani na Muungano wa Ulaya ni maafisa wa ngazi ya juu katika utawala wa jimbo la crimea, rais wa Ukraine aliyengolewa madarakani Viktor Yanukovich, naibu waziri mkuu wa Urusi, wabunge wa Urusi na makamanda wa jeshi.
No comments:
Post a Comment