Thursday, 3 April 2014

CHRISS BROWN AMKUMBUKA EX-GIRLFRIEND WAKE AKIWA JELA

  Chris Brown na Karrueche Tran wanaendelea kuwasiliana pamoja ,hivi karibuni mrembo huyo alimpiga kibuti Breezy baada ya kugundua alikuwa na mawasiliano na wasichana wengine kabla hajatimuliwa Rehab.

Usiku wa jana Karrueche kupitia Instagram alithibitisha kuwa licha ya kuwa hawako pamoja (kama hali ilivyo hadi sasa), lakini bado wawili hao wanaendelea kuwasiliana hasa katika kipindi hiki cha misukosuko aliyonayo Breezy.
Karrueche alirekodi simu ya Chris wakati akitoa ujumbe wake kwa mashabiki wake huku Karrueche akitabasamu, haya ndiyo maneno aliyoyazungumza Chris katika ujumbe huo kwa Fans wake:
“Napiga simu kwa mashabiki wangu wote, kuwajulisha kuwa nawapenda wote, asanteni kwa support yenu. Asanteni kwa kila kitu. Video imetoka naamini mmeifurahia. Na cha muhimu zaidi, K Karrueche, nakupenda”. Alisema Chris
Iangalie Clip ya Karrueche Tran akisikiliza ujumbe huo wa Breezy kupitia Simu yake,

No comments: