Friday, 4 April 2014

MAFIKIZOLO KUTUA NDANI YA BONGO LEO.

Kundi maarufu na mahiri katika muziki wa Kwaito la nchini Afrika kusini, Mafikizolo linatarajiwa kuwasili leo jioni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya onesho moja tu linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Jumamosi ya April 5 2014{Kesho}
.Mafikizolo wamekuwa na rekodi nzuri ya kushinda kwenye tuzo mbalimbali za muziki{Africa}, kutokana na kupiga muziki na kucheza kwa umahiri, hasa mtindo wao maarufu wa Kwaito. Kundi hilo linaloundwa na wasanii wawili, Nhlanhla Nciza na Tebogo Madingoane, kwa sasa Mafikizolo wanaendelea kutamba na vibao vyao viwili matata “Khona” na “Happiness”vinavyosumbua sana kwenye kumbi za burudani kote Africa.

No comments: