Tuesday, 29 April 2014

MHE. MWIGULU NCHEMA AZUNGUMZIA SUALA LA URAIA PACHA KATIKA ZIARA YAKE JIJINI WASHINGTON DC.

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba akihojiana na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production Washington DC.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa anajivunia kiasi cha UZALENDO walichonacho waTanzania hapa nchini, jambo linalompa moyo kuendeleza harakati zake za kusaidia kupatikana kwa uraia pacha, ombi lililo kuu kwa waTanzania waishio nje ya nchi katika mabadiliko ya katiba mpya.
Mhe Nchemba, ambaye alikuwa mmoja wa wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika jijini Washington DC nchini Marekani, amesema kuwa ushiriki wa waTanzania na rafiki zao katika maadhimisho haya, umemdhihirishia nia na mapenzi yao kwa nchi yao, na hilo limemsukuma zaidi kusaidia kupitishwa kwa suala la uraia pacha kwenye katiba mpya

No comments: