Tuesday, 29 April 2014

PICHA-HAFLA YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA VIWANJA VYA IKULU-DAR ES SALAAM.

Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mama Arafa Ridhiwani Kikwete kulia pamoja na ndugu zake.
Mama Arafa Ridhiwani akiwa na ndugu zake katika hafla hiyo.
Wazee wa Politiko Lifo Chipaka na Fahmi Dovutwa kulia wakifurahia Muungano.

Rais  wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete  na Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wakikata keki katika sherehe ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na Mwalimu J.K.Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Aprili 26 mwaka 1964 hafla hiyo ilifanyika juzi kwenye viwanja vya Ikulu na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Seif Ali Idd, Waziri Mkuu Tanzania Mh. Mizengo Pinda na viongozi mbalimbali wa serikali taasisi za dini na vyama vya siasa, Kushoto  ni Mke wa Rais mama Salma Kikwete na kushoto ni Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein
Rais  wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe maalum cha kufyatua mafataki wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.
Wasanii mbalimbali walikuwepo katika hafla hiyo.

Rais  wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete  na Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wakiwalisha keki wake zao katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba akiwa katika picha ya pamoja na Msanii MwanaFA aka Binamu.  

No comments: