Wednesday, 30 April 2014

RAIA WAMKALIA KOONI ZAMARADI KWA KUMHUSISHA MTOTO WA KAJALA KATIKA BIFU LA MAMA YAKE NA WEMA SEPETU.

Zamaradi Mketema
Jambo limezua jambo! Prizenta wa Clouds FM na TV, Zamaradi Mketema yamemkuta  mazito baada ya kumwagiwa mvua ya matusi kisa kikiwa ni kumhoji mtoto wa Kajala Masanja (jina kapuni kimaadili) juu ya ugomvi wa mama yake na Wema Isaac Sepetu.
Wema Sepetu & Kajala enzi za urafiki wao.

Mara baada ya Zamaradi kuzungumza na mtoto huyo kupitia Kipindi cha Leo tena kinachorushwa na Redio hiyo,ndipo mitandao ya kijamii ikalipuka kwa matusi kuwa hakupaswa kumhusisha mtoto huyo kwenye jambo kama hilo.
“Huyu Zama ni....(tusi). Ina maana hajui ....(jina la mtoto wa Kajala) yupo chini ya umri wa miaka 18? Huko ni kumpa mtoto stress tu,” ilisomeka sehemu ya maoni mengi juu ya sakata hilo kwenye mitandao ya kijamii.
Kajala na Mtoto wake.
Baada ya kuona hali hiyo, mwanahabari wetu alizungumza na Zamaradi aliyeonesha kusikitishwa na watu hao huku akifafanua kuwa kilicho mbele yetu ni kutafuta suluhu ya Wema na Kajala, akahoji hayo mengine yametokea wapi?
Hivi karibuni kumeibuka mzozo mkubwa kati ya kundi linalomuunga mkono Wema na lile la Kajala kila moja likilichafua lingine.

No comments: