Saturday, 10 May 2014

KAULI YA SAUTI SOUL BAADA YA KUFUNGIWA VIDEO YAO

Ikiwa inakaribia wiki ya pili sasa tangu kundi la Sauti Soul kuachia video yao mpya ambayo imeleta utata na baadae kutoka taarifa za kufungiwa,hatimae kauli kutoka kwao kama Sauti Soul kuhusu hii video.
Miongoni mwa maoni ya watu kuhusu video hiyo ambayo bado imezua utata na hisia tofauti ni ile hali ya kuonyesha misuli iliyotajwa na mafans wa kike kama jambo la kufurahisha huku upande wa kiume wakisema kama inawadhalilisha.
Kwa mujibu wa bendi nzima la Sauti Soul video ya Nishike ilitungwa tu kwa ajili ya kutuma ujumbe>>’Tuna pitisha ujumbe kwamba wanaume sharti wafanye mazoezi sio tu kupata sixpacks lakini kwa ajili ya afya zao’
‘Wengi wetu wamekua wanene kupita kiwango na njia ya pekee ya kupunguza unene huo nikupitia kufanya mazoezi kwenye gyme’.asema Delvin Mudig ambaye ni miongoni mwa waimbaji wanaounda kundi la Sauti Soul
Katika kauli nyingine Austin Chimano ambaye pia ni member wa Sauti Soul amesema>>’Hatukuiandaa video ya Nishike ili kukera mtu yeyote tunacheza na kuimba Kisauti Soul.tumekua sisi tu.hatukupanga kua na wimbo utakaozua hisia kama hizi Ilikua tu ni dhihirisho la penzi.hakukua na fumbo hapo’.
Naye Bien Aime Baraza ameongezea>>’kama bendi Sauti Soul sasa inawekwa kwenye kiwango sawa na bendi za hadhi ya juu kama P-Square, Mafikizolo,Mikasa na wengine tumekuwa kutoka wakati wa Lazizi na tungependa mafans wetu waendelee kutusapot kutuwezesha kuwa na kujulikana nje ya Bara la afrika’ Mwingine ni Polycarp Otieno ambaye yeye amesema>>’Sanaa inahusu kujieleza na kwetu haikua tu tutoe wimbo ambao watu wangeu skiza na kuridhika,lakini kitu ambacho kingeonyesha hilo kwenye video,ndio tumepata maoni mabaya kutoka kwa wanaume,lakini tunawajibu kua ‘usimchukie mchezaji’, kwa kweli video inayotokea ni ya kuwahamasisha watu wafanye zoezi’.
Iangalie Video hiyo hapo chini,
 

No comments: