Wabunge nchini Uganda wamepitisha muswada unaotoa adhabu kali kwa watu wanaowaambukiza wengine virusi vya HIV kwa makusudi.
Mswada huo unapendekeza adhabu ya kifungo cha hadi miaka 10 gerezani kwa wale watakaopatikana na hatia na pia inapendekeza wanawake wajawazito na wapenzi wao kupimwa virusi vya HIV.
Mbunge mmoja kwa jina Peter Aleper aliambia vyombo vya habari kuwa watu wanaowaambukiza wenzao virusi vya HIV kwa makusudi ni hatari kwa jamii.
"ni lazima waadhibiwe vikali kwa sababu kumuambukiza mtu HIV wakati unafahamu vyema kuwa wewe ni mwathirika ni uuhalifu,'' alisema mbunge huyo. Ni hatari sana kwa sababu mtu huyo anaweza kuichanganya jamii na kumaliza watu kabisa.''
Lakini wafanyakazi katika sekta ya afya pamoja na mashirika ya kutetea haki za wanyonge, wamepinga vikali mswada huo, wakisema kwamba haitafanya lolote kudhibiti ongezeko la visa vya maambukizi.
Wengi wanasema kuwa muswada huo utaongeza tu unyanyapaa kwa watu wanaoishi na virusi hivyo. Pia wanasema kuwa watu watahofia kupimwa kwa hofu ya kutengwa na jamii.
Muswada wenyewe umepitishwa baada ya sheria kali inayopinga vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kupitishwa na rais Yoweri Museveni mwezi Februari mwaka huu.

![]() |
Wanawake wajawazito watalazimika kupima virusi vya HIV pamoja na waume wao |
"ni lazima waadhibiwe vikali kwa sababu kumuambukiza mtu HIV wakati unafahamu vyema kuwa wewe ni mwathirika ni uuhalifu,'' alisema mbunge huyo. Ni hatari sana kwa sababu mtu huyo anaweza kuichanganya jamii na kumaliza watu kabisa.''
Lakini wafanyakazi katika sekta ya afya pamoja na mashirika ya kutetea haki za wanyonge, wamepinga vikali mswada huo, wakisema kwamba haitafanya lolote kudhibiti ongezeko la visa vya maambukizi.
Wengi wanasema kuwa muswada huo utaongeza tu unyanyapaa kwa watu wanaoishi na virusi hivyo. Pia wanasema kuwa watu watahofia kupimwa kwa hofu ya kutengwa na jamii.
Muswada wenyewe umepitishwa baada ya sheria kali inayopinga vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kupitishwa na rais Yoweri Museveni mwezi Februari mwaka huu.
No comments:
Post a Comment