Saturday, 24 May 2014

Moyes achunguzwa na polisi-Uingereza.

Aliyekuwa kocha wa Manchester United David Moyes 
Aliyekuwa kocha wa Manchester United David Moyes anachunguzwa na polisi nchini Uingereza baada ya kushutumiwa kuhusika katika mapigano katika baa moja ya mvinyo iliyoko katika kitongoji cha Lancashire.
Maafisa wa polisi walifahamishwa kuwa saa nne usiku, saa za Uingereza kuhusu tukio ambalo kijana mmoja mteja katika baa ya Emporium iliyoko Clitheroe alidai kapigwa na mtu ambaye ilibainika kuwa ni kocha huyo aliyefutwa kazi wa Manchester United.


Hakuna aliyekamatwa katika tukio hilo huku polisi wakiendesha uchunguzi wao kuhusu nini kilichochea uhasama baina yao wawili.
Watu kadha walioshuhudia wamekuwa wakidai kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 alimgoa kocha Moyes kutokana na matokeo duni ya Manchester United alipokuwa mkufunzi kwa miezi kumi na hivyo kumuudhi sana Moyes aliyemfokea na kumburuta.
Moyes alitimuliwa Old Trafford mapema mwezi huu yapata miezi 10 tangu achukue usukani kutoka kwa kocha mkongwe Sir Alex Fergusson aliyestaafu kuifundisha timu hiyo.
Moye ametokea klabu ya Everton ambayo ameiongoza kwa zaidi ya miaka 10.

No comments: