Mzungu Kichaa atoa single yake ya pili kutoka kwenye CD yake mpya
iitwayo RELAX. Katika wimbo huu amemshirikisha Juma Nature na Karen
Mukupa. Mzungu Kichaa alikuwa na haya ya kusema, "Juma Nature ndiye
aliyenipa jina langu la kisanii nilivyokuwa nikifanya featuring kwenye
nyimbo kadhaa za Bongo Flava mwaka 1999 na 2000. Pia niliweka vocals
pamoja na TID kwenye wimbo wa Nature uitwao Hili Game.
Kwahiyo nina furaha kubwa kupata fursa ya kufanya kazi na Juma Nature tena katika
wimbo huu. Karen Mukupa pia alishawahi kushirikiana na Nature siku za
nyuma na ni rafiki yetu sote wa siku nyingi. Karen ni msanii mkubwa sana
nchini Denmark anapotokea na nimefurahi kuweza kuwashirikisha wote
wawili." Mzungu Kichaa pia alisema kuwa wimbo huu ni kwaajili
ya kujenga umoja ili kufikia malengo na ndoto katika fani ya muziki.
Wimbo huu unazungumza kwa niaba ya wasanii wote wa Afrika Mashariki.
Vocals zimerekodiwa studio ya MJ Records na ngoma imerekodiwa
live ndani ya Caravan Records na Abdalla Membe, Shabani Rashid
(keyboard), Kevin Mpangala (Bass), Mzungu Kichaa (Guitar).
ISIKILIZE/DOWNLOAD HAPA>>> https://mkito.com/sounds/short-clips/1403529385dc912a253d_mkito.mp3

No comments:
Post a Comment