Thursday, 26 June 2014

P-AQUARE WAPIGA COLLABO NA KUSHOOT VIDEO NA T.I

Peter Okoye{Psquare} & T.I
Baada ya Wizkid wa Nigeria kuthibitisha kuwa amerekodi wimbo na muimbaji wa Marekani Chris Brown, kundi la mapacha wa P-Square nao inasemekana kuwa wamefanya collabo na msanii mkubwa wa Marekani T.I.
Kwa mujibu wa mtandao wa Linda Ikeji wa Nigeria, chanzo cha karibu na kundi hilo kimesema P-Square wamerekodi wimbo na rapper T.I na pia Siku ya jana walikuwa Location Wakishoot video ya wimbo huo huko Atlanta, Marekani.
Ingawa bado mapacha hao hawajasema chochote kuthibitisha hilo, lakini Peter Okoye mmoja kati ya Mapacha wawili wanaounda kundi hilo{PSQUARE} ameonekana kwenye picha akiwa na T.I jana na inasemekana picha hiyo ilipigwa wakati wa kushoot video hiyo.


No comments: