Friday, 27 June 2014

PENNY & WEMA WAKUTANA USO KWA USO STUDIO.


Katika hali isiyotarajiwa, mchumba wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Wema Sepetu na aliyewahi kuwa mchumba wa msanii huyo Wa zamani, Penniel Mungilwa ‘Penny’ wakutana studio na kila mmoja kumkwepa mwenzake.
Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Posta, jijini Dar katika Studio za Amaya ambayo ni saluni inayotumika kurekodia vipindi mbalimbali vya Mkasi vinavyorushwa kupitia Runinga ya EATV.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Picha lilianzia kwa muigizaji Aunt Ezekiel kualikwa na mtangazaji wa kipindi hicho, Salama Jabir kwenda kufanya mahojiano, akiwa ameambatana na shosti wake Wema ndipo ghafla wakakutana na Penny ambaye naye alialikwa kwa wakati wake.
Chanzo kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya Aunt na Wema kufika studio hapo, Salama aliwakaribisha na wakaanza kurekodi kipindi hicho, lakini walipokuwa wakiendelea na mahojiano, Penny naye aliwasili bila kujua kama Wema alikuwepo.
“Penny alipofika alizama ndani na kukutana na Salama ambaye alimwambia kuwa kuna watu wanatoka ndani muda si mrefu hivyo wakati bado wanaongea, Wema na Aunt walitoka studio ambapo Penny alikimbilia kwenye gari lake kukwepa kuonana na Wema ambaye pia alionekana kutotaka kuonana na Penny,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Kwa kuwa Wema naye alimuona kwa mbali Penny, alimtaka Aunt waingie kwenye gari fastafasta na kuondoka eneo hilo.”
Mapaparazi wetu baada ya kuunyaka mchongo huo, walimtafuta Penny ili kumsikia anazungumziaje ishu hiyo. Alipopatikana, alijibu hivi:
“Mimi sikumkimbia Wema na itambulike kuwa wakati naenda pale sikujua kama Wema alikuwepo hivyo nilifika na kusubiria muda wangu wa mahojiano nikiwa ndani ya gari, sikuwa na haja ya kujua Wema yupo ama la.”
Jitihada za kumpata Wema hazikuzaa matunda lakini alipotafutwa Aunt Ezekiel, alitiririka:
“Nilimuona Penny kweli pale studio ingawa mwanzo nilitahamaki maana sikujua kama naye alikuwa akisubiria tutoke aingie kwenye kipindi ila Salama alinishtua sana baada ya kusema kabla hatujatoka ndani tusubiri aandae uwanja wa ngumi, alitania.”
Wema na Penny wanadaiwa kuwa picha haziendi baada ya Wema kumtuhumu Penny ambaye alikuwa rafiki yake kutoka na mchumba wake Naseeb Abdul"Diamond Platnumz".

No comments: