Monday, 16 June 2014

STAA WASTARA APINGA MASTAA KUAGWA LEADERS

Wastara Sajuki.
Mkali wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amepinga kitendo cha mastaa wa Bongo kuagwa Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar wanapokutwa na umauti.
Akizungumza na gazeti moja la habari za mastaa na kijamii Bongo, Wastara alieleza kwa huzuni kubwa kuwa hafurahii eneo la Leaders kutumika kuagia kwa sababu ni eneo hilohilo ambalo hutumiwa kwa starehe.
Wastara akiwa kwenye moja ya misiba ya Bongo Movie.
 “Ukweli kwa upande wangu napinga mastaa kuagwa Leaders kwa sababu Leaders mara nyingi hutumika kama sehemu ya anasa. “Ningeiomba serikali itutafutie sehemu maalum kwa ajili ya kufanyia shughuli zote za misiba ya watu maarufu,” alisema Wastara.

No comments: