WATU nane wamekufa kwa kung’atwa na Mbwa wenye Ugonjwa wa kichaa cha
Mbwa Wilayani Songea mkoani Ruvuma, kuanzia mwezi Januari hadi mwezi huu
na wengine 17 kung’atwa na kupata madhara mabalimbali.
Taarifa ya Kaimu Afisa Mipango wa Manispaa hiyo, Gaspar Tillya, iliyotolewa Juni 12, 2014 imesema kutokana na hali hiyo msako mkali umeanza kufanywa ili kuwatafuta Mbwa wenye ugonjwa huo, ingawa msako huo unakabiliwa na ukosefu wa fedha na Wanajeshi wanasaidia kusaka Mbwa hao kutokana na baadhi ya Mbwa hao kuingia kwenye Kambi ya Jeshi ya Changamali ya mjini Songea.
Diwani wa Kata ya Ndilimali Tembo wilayani humo, ambayo ni moja ya Wilaya zilizoathiriwa na Ugonjwa huo, William Kapinda, amesema tatizo la ugonjwa huo ni kubwa kutokana na kung’ata watu wengi ambao wengine bado wanapata matibabu ya kuchoma Sindano.
Hata hivyo, Manispaa ya Songea inayotikiswa na ugonjwa huo, haina dawa za kutibu watu waliong’atwa na Mbwa hao na pia idara yake haina fedha za mafuta kwa ajili ya magari yanayotakiwa kuzungukia na kuua Mbwa wenye ugonjwa huo.
Wilaya ya Tunduru
Zaidi ya Wananchi 17 wakiwemo wanafunzi 3 Wilayani humo, wameripotiwa kung’atwa na Mbwa wenye ugonjwa wa huo na kuwasababishia madhara mbalimbali.
Mganga wa Mifugo wa Halmashauri hiyo, Dk. Frenk Nkoma, amesema hivi karibuni katika Wilaya hiyo kuzuka kwa mlipuko wa ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa Nkoma, maeneo yaliyo athirika na ugonjwa huo ni pamoja na Vijiji vilivyopo katika Kata za Mchoteka, Marumba, na Muhuwesi, na kwamba chanzo cha ugonjwa huo kuenea katika Wilaya yao kilitokana na kuwepo kwa taarifa za kuingia kwa Mbwa mwenye ugonjwa huo kutoka katika Wilaya ya Nachigwea mkoani Lindi mwanzoni mwa mwaka huu.
Amewataja wanafunzi waliodhurika kuwa ni, Ally Kasembe (14), Mussa Sandali (8), na Summa Said (7) wote wakiwa ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Molandi iliyopo katika Kata ya Marimba. Amesema katika matukio hayo watu wengine 10 waling’atwa na kujeruwa vibaya na Mbwa hao na watu 7 waliripotiwa kujeruhiwa katika maeneo hayo na kwenda kutibiwa katika Vituo vya afya, Zahanati na Hospitali zilizopo Wilayani humo.
Takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 55,000 hufariki kila mwaka kutokana na ugonjwa huo kutokana na ugonjwa huo kusababishwa na virusi ambavyo huwapata wanyama na binadamu duniani kote.

No comments:
Post a Comment