Rihanna na Big Sean ni wapenzi! Chris Brown adaiwa kuachana na Karrueche Tran
![]() |
Picha:-Big Sean & Rihanna. |
Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa udaku ‘MediaTakeout’, Rihanna na Big Sean walionekana Jumamosi (July 5) wakiwa katika pool party Ya mchezaji wa NBA, Kevin Durant huko Los Angeles.
Mashuhuda walioeleza kuwa na uhakika walidai kuwa wasanii hao walifika katika eneo hilo kwa pamoja na walikaa na kuishi dakika zote kama couple.
![]() |
Drake"Dreezy" & Rihanna"Riri" |
Wakati Rihanna akiripotiwa kuanza maisha mapya ya mapenzi na Big Sean (kama ripoti ya media takeout itakuwa kweli), Chris Brown yeye anaripotiwa kuachana tena na Karrueche Tran ambaye huwa na maisha ya kuachana na kurudiana mara kwa mara.
![]() |
Karrueche & Chris Brown. |
“Love what you have before life teaches you to love what you lost.” Aliandika Karrueche Tran kwenye Instagram.
![]() |
Picha moja ya Birthday alizowahi kusherehekea Chris Brown akiwa na Karrueche Tran. |
No comments:
Post a Comment