![]() |
| Tim Howard |
Mlinda mlango wa klabu ya Everton ya nchini Uingereza pamoja
na timu ya taifa ya Marekani (USA) Tim Howard, amepata wakati mgumu
wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Los Angeles akiwa sambamba
na kikosi cha The Yanks ambacho kilikuwa nchini Brazil kikishiriki
fainali za kombe la dunia za mwaka huu.
Tim Howard, ambaye ameibuka shujaa wa taifa la Marekani kufuatia uwezo mkubwa aliouonyesha wakati wa The Yanks ikicheza michezo ya fainali za kombe la dunia huko nchini Brazil, alipata changamoto hiyo kufuatia kila shabiki aliyekutana naye uwanjani hapo kutaka kumsalimia na kumkumbatia.
Mashabiki wengine walionekana wakimpiga picha kwa ajili ya kumbukumbu zao binafsi, hali ambayo bado ilionekana kumkera lakini alijitahidi kutimiza shauku za mashabiki hao.
Hata hivyo Tim Haward alipewa tahadhari na raisi wa Marekani Barack Obama kwa kumueleza hali halisi iliyokuwepo nchini humo mara baada ya ujasiri aliouonyesha wakati wa mchezo wa hatua ya 16, ambapo USA walipambana na Ubelgiji na kufungwa mabao mawili kwa moja.

No comments:
Post a Comment