![]() |
| Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Bw,Seleman Kova. |
Dar es Salaam. Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewakamata watu wanane na kati ya hao,
wawili wakidaiwa kuhusika na mauaji ya Sista wa Kanisa Katoliki,
Cresencia Kapuri na wengine, uporaji wa Benki ya Barclays, Tawi la
Kinondoni.
Watuhumiwa
hao wawili wanadaiwa kuwa, Juni 23, mwaka huu walifanya mauaji ya Sista
huyo eneo la Riverside, Ubungo, Dar es Salaam na kupora kiasi cha Sh,20
milioni na nyaraka mbalimbali.
Katika tukio jingine la Aprili 15, mwaka huu watuhumiwa wengine wanadaiwa kupora Sh,500 milioni za benki ya Barclays.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema
majambazi hao walikamatwa kutokana na operesheni kali inayoendelea
jijini hasa baada ya kifo cha sista huyo.
Kamanda
Kova alisema watuhumiwa waliokamatwa kuhusiana na mauaji ya mtawa huyo
wa Kanisa Katoliki, mmoja alikuwa akiendesha bodaboda na alimbeba
jambazi mwenzake akiwa na fuko la mamilioni ya fedha na kutoroka nalo
wakati mtuhumiwa wa pili aliyekamatwa ambaye ni mfanyabiashara, ndiye
aliyekuwa kiongozi katika tukio hilo.
Kova alisema polisi bado inawatafuta watuhumiwa wengine wawili.
Chanzo: Mwananchi

No comments:
Post a Comment