Friday, 4 July 2014

SabaSaba: wasanii wa kundi la 'Original Comedy' wageuka wahudumu wa mgahawa waliouanzisha

Maonyesho ya 38 ya sabasaba yanaendelea katika eneo la Sabasaba, Dar es Salaam. Makampuni, vikundi na watu mbalimbali wamefika kwa wingi kuonyesha bidhaa zao kwa mtindo utakaowawezesha kuwa karibu zaidi na wateja wao.
Kundi la Ucheshi la ‘Original Comedy’ linaloundwa na wachekeshaji kama Joti, Masanja Mkandamizaji, Wakuvanga, Mpoki na Mack Regani limeanzisha mgahawa halisi kwenye maonesho hayo ambapo wasanii wa kundi hilo ndio wahudumu.
Wakizungumza juu ya hilo, wasanii wa kundi hilo wamesema kuwa wamefanya hivyo kwa lengo la kuonyesha biashara yao,Na pia kuwa karibu zaidi na mashabiki wao wakiendelea kuwahudumia na kupiga nao picha kwa muda wote watakaokuwa katika maonyesho hayo hususan watakapotembelea mgahawa wao.

No comments: