Picha
za staa wa sinema na Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole Kiuno’
zinazomuonesha live akiwa chumbani tena kitandani kimahaba na mwandani
wake, Nuh Mziwanda zimevuja, Risasi Jumammosi linazo kwenye makabrasha
yake.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho
ni mtu wa karibu wa Shilole, picha hizo walijipiga wenyewe wakiwa
kitandani nyumbani kwa mwanadada huyo, Kinondoni jijini Dar.
Chanzo hicho kilidai kwamba picha
hizo walijipiga baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani kwani kabla ya hapo wasingefanya hivyo.
Katika picha hizo zinazowaonyesha
wawili hao wakiwa katika mahaba niue, Shilole anaonekana akiwa amemlalia
Mziwanda ambaye naye amejiachia vya kutosha.
Habari za ndani zinadai kwamba mmoja
wa watu wa karibu alishika simu ya Shilole kisha akajifowadia picha hizo
ndiyo chanzo cha kumfikia sosi wetu huyo.
Baada ya kuzidaka picha hizo, gazeti
hili lilimtafuta Shilole ambaye kwa sasa anakimbiza na ngoma yake mpya
ya Namchukua ambapo alipopatikana kwa njia ya simu alisomewa mashitaka
yake ndipo akafunguka namna alivyochezewa na mtu wa karibu yake.
“Kweli hizo picha ni zangu na
Nuh (Mziwanda), tulijipiga kwa ajili ya kumbukumbu na tulikuwa na muda
mrefu hatujajiachia si unajua tena Mwezi Mtukufu?
“Unajua simu yangu haina password na nina watu wengi wa karibu so
nahisi ndiyo wamezivujisha na nikimjua namtoa kabisa kwenye network
yangu maana siku nyingine anaweza kunifanyia jambo kubwa baya.”
Mbali na hilo, Shilole amesema yupo kwenye mazoezi ya kufa mtu
akitamba kwamba atamkimbiza vilivyo staa wa Nigeria, Yemi Alade
watakapokutana jukwaa moja kwa ajili ya shoo kubwa kwenye Tamasha la
Usiku wa Matumaini, Agosti 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
SOURCE-GPL



No comments:
Post a Comment