Wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha North Carolina nchini Marekani, wanatengeza rangi mpya ya kucha ambayo inaweza hubadili rangi katika sehemu yoyote iliyo na madawa ya kulevya yanayotumiwa na wanaume kama mtego kwa wasichana na wanawake kwa ujumla.
Vijana hao wanasema kuwa wanawake hujipata hatarini wanapopelekwa nje au kwenye 'Date' na wanaume wenye nia mbaya nao. Wanasema rangi hii mpya ya kucha itaweza kuonyesha ikiwa kinywaji kimewekwa dawa za kulewesha kama vile GHB na Rohypnol. Lengo la kampuni hio inayomilikiwa na wanafunzi hao ni kubuni teknolojia ambazo zinawapa wanawake uwezo wa kujikinga dhidi ya ubakaji au dhuluma za kingono. Ukarasa wao wa Facebook unasema rangi hiyo ya kucha inaweza kumlinda msichana au mwanamke yeyote kwani anaweza kuingiza kidole chake katika kinywaji alichonunuliwa na mwanamume na kuona ikiwa amewekewa chochote humo kwani rangi hiyo ya kucha inabadili rangi ikiwa kinywaji kile kina dawa za kulevya. Rangi hiyo inatengenezwa na kampuni ya wanafunzi hao inayoitwa....'Undercover Colours' na tayari imependwa sana na maelfu ya watu ilipotambulishwa rasmi kwa ukurasa wa Facebook na Twitter wa vijana hao. Lakini hisia mchanganyiko ndizo zimeshuhudiwa zaidi. Mmoja wa wasichana walioonekana kufurahishwa na ugunduzi huo Adam Clark Estes anayeandikia Gizmodo, alisema kwenye ukurasa wa Facebook wa Undercover colours kwamba, ''kuna vitu vingi vya kuchunguza ikiwa kinywaji cha mtu kimewekwa dawa yoyote ya kulewesha. ''Ila ni vigumu kubeba vifaa hivyo hasa nyakati za usiku unapokuwa umetoka nje na mwanamume. Jessica Valenti anayeandikia jarida la Guardian, alisema ''Nafurahi kuwa vijana hawa wanataka kuzuia ubakaji, lakini kwa kuwa ujumbe huu unaelekezwa kwa wanawake kuwa wajizuie na ubakaji, sio sawa.''
![]() |
| Hii ni moja ya Picha za Wanamitindo nchini India,Picha zinazochochea tabia za kibakaji. |
Source-BBC SWAHILI.
TOA MAONI YAKO HAPA>>>https://www.facebook.com/Ngessakinollo


No comments:
Post a Comment