Tuesday, 2 September 2014

Barnaba na Fally Ipupa Kuachia Ngoma ya pamoja .

Fally Ipupa & Barnaba

Barnaba ambaye ameutaja mwaka huu kuwa ni mwaka wake wa mafanikio zaidi ameelezea mpango wa safari yake kwenda Ufaransa na Marekani mwezi huu. Akiongea na Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm, msanii huyo amesema kuwa safari yake italenga katika kukamilisha collabo yake na Fally Ipupa pamoja na video lakini pia ataenda New York kwa ajili ya mradi wa Malaria No More. “Panapo majaliwa katikati ya mwezi ujao naenda Ufaransa. Nikitoka Ufaransa narudi tena New York na baada ya hapo narudi Dar. Kwa ajili ya wahalade lakini pia kwa ajili ya project nyingine. Kwa sababu mimi pia ni balozi wa malaria no more, kwa hiyo naenda kama balozi ambaye naenda kuchukua elimu kidogo.” “Lakini Ufaransa naenda kwa ajili ya Fally Ipupa. Naenda kufanya collabo nae na wimbo wangu pia nafanya nae. Huo wimbo ulifanyika ulikuwa nusu yeye hakumaliza. Kwa hiyo inabidi nimfuate kule tumalizie . Masters nitafanyia kulekule na video pia nitafanyia kule panapo majaliwa.”

No comments: