| Mama Diamond,Diamond & Wema. |
NI Gumzo! Hiyo ndiyo kauli pekee inayoweza kuakisi pati ya kuzaliwa ya supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ametimiza umri wa miaka 25, iliyofanyika usiku wa juzi kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower (PSPF), Posta jijini Dar,
Ubavu wa Diamond, Wema Isaac Sepetu ‘Onyinye’ ndiye aliyekuwa gumzo katika sherehe hiyo baada ya watu wengi kuwa na shauku ya kuona kama atafika au la. Wengi walitaka kujua kama atafika, ataingia kwa staili gani kutokana na minong’ono iliyokuwa ikiendelea kuwa huenda Wema asitokee kwenye sherehe hiyo kutokana na madai kuwa Diamond alikasirika baada ya kukuta mpenzi wake huyo amezawadiwa ndinga aina ya BMW 454i na Martin Kadinda hivyo kuhoji uhalali wake.
Katika hali isiyotegemewa, Diamond na Wema waliingia pamoja huku wakiwa wameshikana mikono. Wema alivaa gauni lenye mpasuo wa aina yake, kila mmoja alimfuatilia hatua kwa hatua kutaka kujua atasababisha tukio gani. Watu kibao waliohudhuria ukumbini hapo, walipiga shagwe za kutosha kwa Wema huku wakidai ndiye mke halali wa Diamond hivyo kumshangilia kila alipokuwa akiinuka kufanya tukio.Kwenye ukumbi huo, kila kitu kilikuwa kimeshalipiwa hivyo waalikwa wote walikunywa, kula na kucheza kwa gharama za Diamond.
Pia kulikuwa na bendi mbalimbali zilizotumbuiza hasa Ya Moto Band na wasanii mmojammoja au kundi huku kukiwa na mastaa wengi wa filamu na muziki Bongo ambao walibaki midomo wazi kutokana na namna shughuli hiyo ilivyokuwa kubwa.na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa;
SAA 5:00 USIKU SHILOLE, NUH FULL MAHABA
Shilole na Nuh Mziwanda wakiwa wameongazana wanaingia ukumbini nakwenda kuketi full mahaba au mahaba nikongorowe, kila mmoja anamdekeza mwenzake.
| Nuh Miwanda & Shilole |
Diamond na ubavu wake, Wema au Madam ndiyo wanaingia kwa staili ya kumbikumbi. Pembeni yao mama Diamond naye anawapa kampani. moja kwa moja Diamond anafikia kufungua shampeni, waalikwa full kelele.
SAA 6:20 USIKU NGOMA ZA ASILI
Sasa ni zamu ya ngoma za asili zinapigwa…Duh! Mzuka umempanda Diamond ameinuka ameanza kucheza na Wema. Waalikwa full kushangilia, wanaonesha kuzirudi ngoma za asili hatari.
Hapa wasanii kibao wameanza kutoa shangwe, namuona Vincent Kigosi ‘Ray’, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Queen Darlin, Petit Man, Chegge, Temba, Yamoto Band, Jacob Steven ‘JB’ na Aunt Ezekiel wanakula bata.
| Wasanii Richie Mtambalike,Ray Kigosi ,Irene Uwoya & Jacob Steven{Jb} |
SAA 7:00 USIKU KEKI YAKATWA
Keki ndiyo inakatwa, Diamond amekata, anaanza kuwalisha wageni mbalimbali. Ameanza mama Diamond, amefuata Wema sasa.
Keki kubwa zipo tatu, shampeni zipo zaidi ya kumi. Keki ndogo ndiyo zipo za kumwaga, hazina idadi.
![]() |
| Diamond akimlisha keki Said Fella kwa niaba ya Menejimenti yake. |
| Ma Mc wa shughuli nzima CHIDI BEENZ & SAUDA MWILIMA. |
| Wageni waalikwa wakiendelea kuingia ukumbini hapo. |
| Gari aina ya BMW-X6 aliyozawadiwa Diamond na Menejiment yake. |
| Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria Shughuli hiyo. |

No comments:
Post a Comment