![]() |
| Davido |
Msanii wa Nigeria anayetamba na hits kibao, Davido ataingia Tanzania mwishoni mwa mwezi huu na kufanya show kubwa November 1. Msanii huyo anayeletwa na kituo cha radio cha 100.5 Times Fm kupitia tamasha lake jipya lililopewa jina la ‘The Climax’. Ikiwa tayari vidokezo vya show hiyo vimeanza kurushwa hewani kwenye kituo hicho cha radio huku orodha ya mengi yatakayofanyika ikitarajiwa kuwekwa wazi muda wowote kuanzia leo. Davido ambaye ni mshindi wa tuzo kadhaa kubwa ikiwemo tuzo ya BET na MTV (MAMA) anatamba na hits kadhaa ikiwemo Skelewu, Aye, tchelete na nyingine nyingi. Hivyo mbongo Kaa mkao wa kushangweka na kilele cha burudani cha mwaka ‘The Climax’ ya 100.5 Times FM.Muziki Wetu- Afrika Yetu...................
“Paris was Great next stop!! LONDON –LAGOS-WARRI-SOUTH AFRICA-NAMIBIA-TANZANIA lego.” Hii imeandikwa na Davido mwenyewe kwenye mtandao Instagram.

No comments:
Post a Comment