Monday, 6 October 2014

Mourinho: Kilichotokea Kinapaswa Kusahauliwa, Sina Tatizo Na Wenger (Video)


Kwa upande wa Jose Mourinho amesema hana budi kusahau kilichotokea uwanjani kutokana na kuamini kwamba kilichopita hakina nafasi ya kujadiliwa mbele ya waandishi wa habari ambao walitaka kusikia chochote kutoka kwake. Amesema yapo mengi yaliwahi kutokea uwanjani dhidi yake na aliyachukulia kawaida hivyo kwa tukio lililomsibu hapo jana nalo analiona kama sehemu ya yale yaliyopita, kutokana na kwenye soka kuna mambo mengi hutokea bila kutarajiwa. Amesema tukio la kusukumwa na Arsene Wenger halimaanishi kama ana tatizo na mzee huyo kutoka nchini Ufaransa, zaidi ya kuamini lilitokea kwa bahati mbaya.

Jose Mourinho on clash with Arsene Wenger during Chelsea v Arsenal - "It's no problem"

Kitendo cha Arsene Wenger kumsukuma Jose Mourinho ambacho kiliwastaajabisha waliokuwa wanafuatilia mpambano huo uliounguruma kwenye uwanja wa Stamford Bridge kiliingiliwa kati na muamuzi wa akiba Jon Moss.

Arsene Wenger VS Jose Mourinho FIGHT Scene


Katika mchezo huo Arsenal walikubali kichapo cha mabao mawili kwa sifuri yaliyofungwa na Eden Hazard kwa njia ya Penati pamoja na mshambuliaji kutoka nchini Hispania Diego Costa. Matokeo ya michezo mingine iliyochezwa jana nchini Uingereza:
Man Utd 2 - 1 Everton
Chelsea 2 - 0 Arsenal
Tottenham 1 - 0 Southampton
 West Ham 2 - 0 QPR

No comments: