Thursday, 16 October 2014

T.I KUZINDUA PAMBA ZAKE KWENYE MSIMU WA SERENGETI FIESTA-2014.

T.I
Baada ya Kampuni ya Clouds Media ambao ndio waratibu wa Tamasha la Fiesta,kumtangaza Mshindi wa Tuzo za Grammy 2014,Msanii T.I toka nchini Marekani kama ndiye msanii wa Kimataifa atayetoa burudani siku ya kilele cha Tamasha hilo tarehe 18th-October-2014,Siku ya Jumamosi ya wiki hii,ndani ya Viwanja vya Leaders Club{Kinondoni}.
Taarifa za ndani ya kampuni hiyo zinadai kuwa,zaidi ya burudani kali ya Hiphop itakayoshushwa stejini na mkali huyo toka Click yake ya The Hustle Gang,pia anatarajia kutambulisha Pamba zake siku hiyo hiyo ya tarehe 18th,Oct ndani ya duka maarufu la Pamba jijini dar es salaam THE POP UP SHOP,duka lililopo ndani ya Supermarket ya DAR FREE MARKERT,
Akizungumzia uzinduzi wa Pamba hizo Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Grand Hurstle Records Kampuni mama ya The Hurstle Gang,Jason Geter ambao ndio wanaomsimamia msanii B.O.B na mwanadada anayekuja kwa kasi kwenye Anga la Muziki wa Hiphop Iggy Azalea wana imani kubwa na soko la bidhaa zao katika ukanda huu wa Africa hasa Africa ya Mashariki.
Siku hiyo ya tarehe 18th Oct duka la POP UP SHOP litafunguliwa mapema kuanzia saa Nne asubuhi ambapo wateja watapata nafasi ya kujinunulia Pamba hizo Aina ya Akoo,Strivers na Row Clothes,wakati wafanyabiashara wakubwa wenye maduka nao watapata nafasi ya kutoa Oda zao pia.

No comments: