CHIDI BEENZ...Akionyesha mkono kupinga kupigwa picha.KESI ya msanii
muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro ’Chid Benz’, imeahirishwa tena
leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi Desemba Mosi mwaka huu.
Msanii huyo anakabiliwa na kesi ya kukamatwa na madawa ya kuletvya
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jiji Dar es
Salaam wakati akisafiri kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya kutumbuiza.
Upande wa mashitaka ukiongozwa na mawakili wawili Ofmed Mtenga na
Leonard Challo mbele ya Hakimu Waliarwanda Lema, umesema upelelezi bado
haujakamilika nakutaja tarehe ya kusikilizwa kesi hiyo Desemba mosi.
|
No comments:
Post a Comment