Monday, 26 January 2015

RAIS KIKWETE AWASILI RIYADH KUHANI KIFO CHA MFALME WA SAUDI ARABIA, KUFANYA ZIARA YA KIKAZI UJERUMANI NA UFARANSA

PICHA:-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
 Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kijeshi mjini Riyadh,
Nchini Saudi Arabia,  asubuhi ya Jana, Jumapili, Januari 25, kuhani Msiba wa kifo cha
Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud
 aliyefariki Alhamisi na kuzikwa
Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba huo wa Mfalme Abdullah,
Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na
Ufaransa kwa ziara za kikazi.

 ambako Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili kesho, Jumatatu, Januari Ishirini na Sita, akitokea Riyadh, Saudi Arabia, anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) ambako viongozi mbali mbali duniani watajadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.

Baada ya kumaliza ziara yake Ujerumani, Rais Kikwete atakwenda Ufaransa ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ufaransa. Aidha, Rais Kikwete atafungua jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa na pia nyumba ya balozi.

Rais Kikwete baada ya kumaliza ziara zake za kikazi katika nchi za Ujerumani na Ufaransa atakwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu – Dar es Salaam. 25 Januari, 2015

No comments: