Baada ya Mbatia kuleta hoja ya dharura juu nguvu
iliyotumiwa na polisi kwenye maandamano ya CUF jana tarehe 27 January
ili ijadiliwe na wabunge kama hoja ya dharura, spika Makinda aliamuru
serikali ilete majibu kesho ndio ijadiliwe.
Wabunge walisimama kushinikiza hoja ijadiliwe lakini Makinda aliendelea na msimamo wake wa hoja kujadiliwa kesho baada ya Serikali kuleta majibu, hapo ndipo sintofahamu ilipozidi na kuleta kutoelewana kati ya wabunge wa Upinzani na Spika. Ilibidi spika Anna Makinda kuahirisha bunge mpaka kesho lakini baadae akabadili na kusema saa kumi jioni leo hii.

No comments:
Post a Comment