PICHA-Mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel wakiangusha kicheko katika kaburi la marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’.
INAWEZEKANA ilikuwa utani? Au ‘waliamka’ nazo?! Kweli binadamu anaweza kuvunjika mbavu (kicheko) juu ya kaburi la mpendwa wake? Mh!Lakini imetokea! Wakati dunia ikisherehekea ujio wa mwaka mpya wa 2015, mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel walionyesha jambo tofauti kufuatia kutinga kwenye kaburi la aliyekuwa nyota wa Bongo Fleva, marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ na kutumia muda mwingi kucheka na kutuma meseji kwa simu wakiwa juu ya kaburi hilo.
INAWEZEKANA ilikuwa utani? Au ‘waliamka’ nazo?! Kweli binadamu anaweza kuvunjika mbavu (kicheko) juu ya kaburi la mpendwa wake? Mh!Lakini imetokea! Wakati dunia ikisherehekea ujio wa mwaka mpya wa 2015, mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel walionyesha jambo tofauti kufuatia kutinga kwenye kaburi la aliyekuwa nyota wa Bongo Fleva, marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ na kutumia muda mwingi kucheka na kutuma meseji kwa simu wakiwa juu ya kaburi hilo.
Tukio
hilo lililonaswa zimazima na kamera zetu lilijiri
Januari Mosi, mwaka huu kwenye kaburi la Ngwea lililopo katika Makaburi
ya Kihonda mjini Morogoro.
ILIVYOKUWA
Aunt
ndiye aliyeanza kutia timu kwenye makaburi hayo na kukaa. Baadhi ya
‘kruu’ ya Wema, akiwemo Petit Man nayo ilifika na kuungana na Aunt.Baada
ya dakika tatu, Mama la Mama, Wema aliwasili akiwa ndani ya nguo
isiyokuwa ya mtoko, akakaa upande wa pili wa kaburi. Yeye na Aunt
walikaa kwa kupeana ubavu.
Awali
ilidaiwa kuwa, kruu hiyo ilipanga kuwa baada ya kufika kwenye kaburi
hilo wangefanya dua fupi kwa ajili ya kumwombea marehemu apumzike kwa
amani huko aliko.Lakini cha ajabu, kabla ya ibada hiyo, Wema, Aunt na
wafuasi wao walikuwa wakipiga stori za hapa na pale na katika hali ya
kushangaza zaidi, ilifika mahali wakaanza kucheka kile kicheko cha
kuvunjika mbavu bila shuhuda wa tukio hili kujua nini hasa kilichokuwa
kikiwachekesha!
Baadhi
ya wapita njia waliokuwa wakikatiza karibu na makaburi hayo, nao
walipigwa na butwaa kuwaona watu hao, walioamini ni ndugu wa marehemu,
wakiangua vicheko kama hawana akili nzuri. kwa nukta kadhaa walisimama
na kushangaa kabla ya kuendelea na ‘hamsini zao’.-
WEMA ATUMIA SIMU KUFICHA USO
Ni
dhahiri kuwa, Wema alijishtukia kuwa kitendo cha kucheka juu ya kaburi
hakikuwa na ujazo wa kiungwana hivyo haraka sana aliweka simu sehemu ya
midomoni na kumfanya asionekane kwenye kamera kwamba alikuwa akicheka.
Miwani ya jua aliyovaa pia ilimsaidia.
Wakati
Wema akionyesha ubinadamu huo, ‘mwenzangu na mimi’, Aunt yeye
alijimalizia kiu yake ya kicheko mpaka pale alipoamua mwenyewe kuacha na
si kwa kuogopa kamera wala malaika waliolizunguka kaburi lile (kama
wapo) la mmoja wa marapa bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania.
WEMA AJIELEZA
Baada
ya wote kuacha kucheka na kila mmoja kuchukua nafasi ya ubinadamu,
paparazi wetu alimuuliza Wema ni kwa nini walionyesha kuwa na furaha juu
ya kaburi la staa huyo.Wema: “Tumepita hapa ili kumuombea ndugu na
rafiki yetu Mangweha hivyo hatuna lengo lingine zaidi ya hilo.“Ishu ya
kupiga stori na kucheka, tusingeweza kuacha kuongea eti kisa tupo
kaburini, maana kila kitu lazima kijadiliwe hata kukaa hapa tumekaa kwa
sababu tunafarijika kuona kaburi la mwenzetu.”
KWA NINI WALIFANYA ZIARA KABURINI KWA NGWEA?
Awali,
mastaa hao na wapambe wao walikuwa na shoo ya kuukaribisha Mwaka Mpya
iliyofanyika Desemba 31, 2014 ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge mjini
Dodoma.Wakiwa wanarudi Dar, walipiga kituo mjini Morogoro ambapo
miongoni mwa mambo waliyokuwa nayo kwenye ratiba ni kulitembelea kaburi
la Ngwea na kuangusha dua fupi.
Hata
hivyo, baada ya yote hayo, kundi hilo la Wema na watu wake atimaye
walifanya dua fupi ya kumuombea malazi mema Albert Mangweha.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Mangweha
alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Akiwa na miaka 31 alifariki dunia, Mei
28, 2013 nchini Afrika Kusini. Chanzo cha kifo chake inadaiwa ni
matumizi yaliyopitiliza ya madawa ya kulevya. Alizikwa Morogoro,
Tanzania, Juni 6, 2013.
No comments:
Post a Comment