Friday, 27 February 2015

Breaking News:-Ndege ya Jeshi yaanguka na kuwaka moto uwanja wa ndege Mwanza, rubani anusurika!

Taarifa kutoka Mwanza Airport ni kuwa kuna ndege ya Jeshi ambayo hubeba mabomu, iliyokuwa kwenye mazoezi ya kawaida imelipuka na kuteketea.
- Ndege hiyo ilikuwa na Rubani peke yake,
Rubani wa ndege hii, ndg Peter Augustino alifanikiwa kuruka kwa parachuti na kunusurika kufa ingawa inadaiwa amevunjika mguu na kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi .
NB;-RIPOTI ZA WANAHABARI JUU YA TUKIO LENYEWE

Quote By bhageshi View Post
Ni kweli imeanguka na kulipuka moto.

Ni ndege ya Jeshi ambayo hubeba mabomu, ilikua kwenye mazoezi ya kawaida ambayo hufanyika mara kwa mara. Lakini kwa leo haikuwa na mabomu na ilikuwa na Rubani pekee.

Rubani amenusurika kwani aliruka na mwavuli, amepata majeraha kidogo na kukimbizwa hospital ila ndege yote imeteketea kwa moto
.
 
 
By Moshe Dayan View Post
QuoteNi jet fighter, ilikua kwenye routine exercise za kila wiki. Zilikuwa zinaruka mbili kwa formation. Wakati zina take-off moja ikaanza kuwaka moto nyuma. Rubani alitoka kwa ejector seat, amepona. Ndege imeharibika vibaya.
Moshe Dayan.
TAARIFA ZAIDI ZINAFUATA........
 
Source-Jamii Forum,

No comments: