Aunty Ezekiel & Moses Iyobo. |
Baada ya hapo juzi Waziri Lazaro Nyalandu kupitia Clouds FM kukanusha tuhuma zilizokuwa zimezagaa kwenye magazeti na mitandaoni za kuwa anachepuka na mwigizaji wa filamu hapa bongo, Aunty Ezekiel na kusisitiza kuwa yeye sio muhusika wa ujauzito wa mwigizaji huyo, nikaamua kupitapita kwenye kurasa za mcheza shoo wa Diamond, Moses Iyobo ambaye ndio anasemekana kuwa yeye ndio amempa ujauziko mwigizaji huyo. Kwanza nilikutana na andiko la malalamiko kutoka kwa Iyobo, ambaye alikuwa ameweka picha ya Aunty na kuandika haya; “Kama kumpenda nampenda sana lakini kinacho nipasua kichwa mie kuni save dalali kwenye cm yake yani sielewi ata kidogo” Lakini kilichonipa faraja ni picha hiyo hapo juu akiwa na Aunty kitandani na kuandika ule msemo kutoka Yamoto Band ambao unamaanisha mtu akipenda amependaaa. ‘Nzi kufa kwenye kidonda sio ufala ila..........’ Kwa picha na ujumbe huu ni wazi Iyobo ndio baba kijacho kutoka kwa Aunty Ezekiel.
No comments:
Post a Comment