 |
| Producer Sappy |
Producer Sappy ndiye Producer ambaye aliproduce ngoma Namba Moja kwenye Chart za 20 Bora za
Mambo Jambo Radio Arusha kwa wiki iliyopita
XO ya
JOH MAKINI.
Huyu ni kijana wa Kitanzania ambaye amejipatia Umaarufu wa Kupika
Midundo ya Tofauti sana ya Muziki hapa Afrika Mashariki. Sappy amefanya
kazi na Wasanii Kibao hadi sasa Kama Prezzo ambaye alimuundia ngoma ya
Marry Marry na My Girl, Kafanya Kazi na Kaka Sungura Rabbit, Nazizi na
Wasanii wengine Kibao wa Kenya.
Heshima Kubwa sana aliipata kupitia ngoma ya Budder than Most ya
Redsun ambayo Remix yake alishirikishwa Mkali Demarco toka Jamaica na
sasa Heshima ya Sappy kwa Tanzania imeongezwa na XO Ngoma kali toka kwa
joh Makini akishirikishwa Baba Samantha GNako.
 |
| Producer Sappy & Joh Makini. |
Akiongea na @DJHAAZU ndani ya Kipindi cha
Dundo cha
Mambo Jambo Radio
Mapema Leo Sappy ameelezea Historia yake hadi kuja Kufanya kazi na
Weusi wasanii ambao anasema Alikuwa na ndoto ya kufanya nao Kazi toka
kitambo sana.
Sappy alienda Kenya Kusomea Muziki akiaamini kuwa Muziki unahitaji
Elimu zaidi ya ambavyo watu wanafikiria na Alivyoenda Kenya Kusoma
akagundua kuwa Muziki Unavyofanywa Kenya unafanywa Kisomi Zaidi tofauti
na Tanzania.
 |
| Sappy & Prezzo |
Katika Mazungumzo yake akatiririka Mengi haswa alivyokuwa akitamani Siku
moja afanye Kazi na Vijana ambao anaamini Wanajitambua na wanajua
wanachokifanya
WEUSI
 |
| Sappy & Redsan |
KAMA UNA KUMBUKA SAPPY NA MSANII NAZIZI walishaingizwa kwenye
Kashfa ya Kutoka pamoja namaanisha kuwa ilisemekana ni wapenzi Taarifa
zikasema Sappy kathibitisha Ila kwenye Dundo la Mambo Jambo Radio
Ulipata kumsikiliza Nazizi akikanusha hayo na kusema kwamba Sappy ni
Producer kwake, Ni rafiki wa Karibu kama ndugu na kwamba hakuna Mambo ya
Mapenzi
 |
| Sappy & Naaziz |
Endelea kufuatilia hapa Kujua Mengine aliyoyaongea Producer Sappy
No comments:
Post a Comment