Saturday, 14 February 2015

SUPER STAR STARA THOMAS AFUMANIWA


HAYA ni madai mazito! Kwamba, staa wa Bongo Fleva ambaye juzi kati alinusa kwenye gospo ‘ikamshinda', Stara Thomas anadaiwa kufumaniwa na mumewe, Raumu Ally mpaka kufikishana polisi, Risasi Jumamosi halipitwagi na ‘ubuyu’. Kwa mujibu wa shuhuda wa kuaminika, tukio hili lilijiri hivi karibuni nyumbani kwa familia hiyo, Tabata jijini Dar es Salaam. Akilisimulia Risasi Jumamosi baada ya kuulizwa kama kweli fumanizi lilikuwepo, mume wa Stara alifunguka hivi: “Ni kweli ilitokea. Siku ya fumanizi nilikuwa nimesafiri, lakini nikarudi ghafla bila kumpa taarifa mke wangu. “Nilikuwa nyumbani, yeye hakuwepo. Saa 9:00 usiku ndiyo nilimwona Stara akirejea tena akiwa amelewa. Aliletwa na gari mpaka nje ya nyumba.” “Lile gari lilisimama zaidi ya nusu nje bila kushuka mtu ndipo nikaamua kulifuata. Stara aliponiona akamwambia dereva ambaye najua ni jamaa yake, aondoe gari kwani mimi ni mume wake nitampiga. “Nilizuia wasitoke, yule jamaa akarudi nyuma na kuniparuza kwenye mguu na tairi, nikadondoka. Niliposimama nikaokota jiwe na kulirushia gari nikavunja kioo cha mbele.

No comments: