KIUNGO mshambuliaji wa
kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa ‘Anko’ amesaini mkataba wa
miaka minne wa kuitumikia klabu ya Free State Stars ya Afrika kusini.
Mtandao wa michezo wa Bin Zubeiry umeripoti kuwa Ngassa amesaini mkataba huo leo nchini Afrika kusini baada ya kufikia makubaliano.
“Sasa najiandaa kwa maisha
mapya baada ya kucheza Tanzania kwa muda mrefu, hii ni changamoto mpya
kwangu, mpira wa Afrika Kusini upo juu sana ukilinganisha na pale kwetu
(Tanzania). Nataka kutumia fursa hii kuitangaza soka ya Tanzania, ili
klabu zisijifikirie tena kusajili wachezaji wa Tanzania,”Ngassa
amekaririwa na Bin Zubiery leo asubuhi nchini Afrika kusini baada ya
kusaini mkataba wa miaka 4 kuichezea timu ya Free State inayoshika nafasi ya 9 katika ligi kuu nchini humo.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa
timu hiyo maarufu kama Ea Lla Koto, Mmalawi Kinnah Phiri amesema kwamba
amekuwa akimpenda Ngassa kwa muda mrefu na kukutana naye FS ni kutimia
kwa ndoto zake za kufanya kazi na kijana huyo siku moja.
No comments:
Post a Comment