Tuesday, 12 May 2015

KAJALA APIGWA CHUPA USONI.

Kajala Masanja.
Staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja anaendelea vizuri baada yakupigwa chupa na kijana mmoja usiku ya kuamkia jana wakiwa kwenye show ya mwanamziki Mabeste aliyoiandaa ili kuchangisha pesa kwa ajili ajili ya matibabu ya Mkewe.
Leo kupitia ukurasa wake mtandaoni, kajala ameweka picha hiyo hapo juu  na kuandika  “Maisha yanaendelea au sio......” kuonyesha kuwa yupo poa na anaendelea na maisha yake yakawaida.
Akilezea tukio hilo la kupigwa na chupa hapo jana alipofanya mahojiano na mtangazaji Millard Ayo wa Clouds FM kajala alieleza
“Mpaka tumemaliza show, sasa kwenye muda wa kuondoka nikamwambia Meneja wangu amuite msanii wetu mmoja anaitwa Tausi ili tuondoke, sasa wakati nataka kushuka kwenye gari natembea tu sijui chochote nikashangaa chupa imenipiga usoni, nikadondoka na kubiringita kwenye zile ngazi, kuna mkaka na mdada wakaniona wakanisaidia”
Akaongeza kuwa;
 “Aliyenipiga na hiyo chupa ni Mwanaume, simjui na wala sijawahi kumuona hata mara moja…. amekamatwa yuko Osterbay Polisi, nilivyotoka Maisha Club nilipelekwa Hospitali Mwananyamala nimeshonwa usoni aliponiumiza, tukarudi Polisi nikaandika maelezo”.
Pole sana Kajala

No comments: