Thursday, 14 May 2015

Wakuu wa nchi za jumuia ya Afrika Mashariki walaani kupinduliwa serikali ya Nkurunziza Burundi.


Wakuu wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki wamelaani vikali jaribio la mapinduzi yaliyotaka kufanyika nchini burundi huku wakitaka utawala wa sheria kwa kuheshimu katiba na makubaliano ya arusha pamoja na kusogezwa mbele. Akisoma maazimio ya mkutano huo mwenyekiti wa jumuiya hiyo Rais Jakaya Kikwete amesema wanatambua hali ya kisasa iliyotokea burundi na hivyo wanasisitiza makubaliano ya Arusha yaheshimiwe.
Mkutano huo umekubaliana kwa pamoja uchaguzi wa burundi usogezwe mbele hadi hali ya siasa itakapotengemaa. Tofauti na matarajio ya wengi Rais Pierre Nkurunziza hakuweza kuhudhuria mkutano huo licha yakuwepo taarifa kuwa aliwasili jijini Dar es Salaam. Hata hivyo mkutano huo haukuweza kufanyika katika utaratibu ambao umepangwa kufuatia kuwepo kwa taarifa ya kuwepo mapinduzi nchini Burundi ambapo taarifa hizo zimeibua taharuki na wasiwasi miongoni mwa washiriki wa mkutano huo wakiwemo viongozi kutoka nchi wanachama.

No comments: