Thursday, 25 June 2015

FAIZA AJIDHATITI KUMRUDISHA MWANAE KWENYE HIMAYA YAKE.

Faiza Ally.
Kufuatia Hukumu iliyotolewa juzi na Mahakama ya mwanzo Manzese jijini Dar es salaam,Hukumu iliyompa mamlaka mbunge wa Mbeya Mjini{Chadema}Bw,Joseph Desderius Mbilinyi"Sugu"kumlea mwanae akiwa mikononi mwake baada ya kilichohukumiwa kwenye kesi hiyo,kudai mama mzazi wa mtoto huyo,Binti Sasha Desderius hakuwa akimlea kimaadili mema mwanae huyo kwa kipindi chote alichokuwa naye,kwa ushahidi wa picha ulioambatanishwa Mahakamani hapo na Baba mzazi wa Sasha,Bw Sugu{Mb},picha zilizoonyesha ukiukwaji wa maadili kimavazi kwa mama mzazi wa mtoto Bi,Faiza Ally,
Sasa leo kupitia ukurasa wake wa facebook Bi,Faiza Ally ameonyesha ungangari katika safari yake ya kumrudisha mwanae huyo kwenye himaya yake kama alivyokata shauri baada ya maamuzi ya kesi kuamuliwa,
Sasha Desderius Mbilinyi.

Na Hiki ndicho Bi,Faiza Ally alichokiandika kuhusiana na hilo,
NASITIKISHWA SANA NA MANENO YENU MAKALI HASA NYINYI MNAO SAMBAZA KASHFA JUU YANGU KUHUSU MAVAZI YANGU- HAKUNA HIYO SHERIA TANZANIA INAYOSEMA NIPOKONYWE MTOTO KUHUSU MAVAZI YANGU- NIMEKATA RUFAA NA NAWAHAKIKISHIA NITASHINDA KESI NA NITAMLEA MWANANGU NA NITAVAA MAVAZI YANGU NA NITA ENJOY MAISHA YANGU/ NINA MWANASHERIA MAKINI ALIYESOMEA SHERIA NA SI NYINYI MNAO NIPA HUKUMU HUMU NDANI NA KWINGINE! PAMOJA NA MAVAZI YANGU MIMI NI MAMA BORA! MNAJUA UPANDE WANGU LKN HAMJUI UPANDE WA SUGU NA HAKIKA MENGI MTAYAJUA KUPITIA KESI HII/ MAVAZI YANGU NAYAPENDA NA KWA MUJIBU WA SHERIA SI KITU KITACHO NIFANYA NI POKONYWE MTOTO WANGU- MANENO YENU MACHAFU DHIDI YANGU YANANIUMA SANA LAKINI KAMWE HAYATA NIRUDISHA NYUMA KATIKA KUTETEA HAKI YANGU! NAMJUA SUGU NA NINAJIJIUA MM KTK UBORA WANGU KATIKA MALEZI YA MWANANGU/ MM NI MAMA NA SI MAMA TU NI MAMA BORA KWA SASHA NA ANANIHITAJI NA SITAMUACHA NA NYINYI WAJINGA WACHACHE ENDELEENI KUNIPONDA NA KUONA NA STAHILI KUPATA PIGO HILI NA SI WOTE- KUNA WENGINE WEMA KWA UPANDE WANGU NA WASHUKURU NA NINA WAAHIDI SITAWARUDISHA NYUMA NITASIMAMA MPAKA KIELEWEKE- SASA HIVI NI JASIRI KUPITA MAELEZO
                              💪.....IN GOD WE TRUST INSHAALLAH

No comments: