Tuesday, 23 June 2015

NAPE MNAUYE:-CCM ITASHINDA TU HATA KWA GOLI LA MKONO

Nape Mnauye.
CCM imesema kuwa itahakikisha inarudi Ikulu hata “kwa bao la mkono” wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25. Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya Nyehunge wilayani Sengerema.

“Rangi inayoenda Ikulu ni hii (anaonyesha shati lake la kijani ambayo hutumiwa na chama hicho). Tuna uhakika na ushindi wa Rais. Kwa namna yoyote ile, CCM itarudi Ikulu hata kama ni kwa bao la mkono... bao ni bao tu ili mradi refa hajaona,” 

Source: MCL

Nini maoni yako kutokana na kauli hii ya Nape?

FUNGUKA HAPA>>>>https://www.facebook.com/Ngessakinollo

No comments: