![]() |
| Papaa Msofe. |
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemfutia kesi ya Mauji iliyokuwa ikimkabili mfanyabishara maarufu Marijani Abdubakari Msoffe baada ya kupokea taarifa toka kwa MKurugenzi wa Mashitaka (DPP) , Biswalo Mganga Leo Kuwa Hana nia ya kuendelea kumshitaki tena.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 ,inampa mamlaka DPP kuifuata kesi ya jinai bila kuhoji wa na mtu yoyote wala mamlaka yoyote ile. Hata hivyo dakika Chache baada ya Kufutiwa Kesi hiyo ya mauji kinyume na Kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002 ambapo kisheria Mahakama ya Kisutu ilikuwa haina mamlaka ya kuisikiliza na haina dhamana na hivyo kwa Kipindi chote hicho tangu Agosti 10 Mwaka 2012 hadi Leo alikuwa akiishi Gereza la Keko Kisha aamishiwa gereza la Ukonga .
Leo pia upande wa Jamhuri umemfungulia Kesi moja ya kughushi Nyaraka za Viwanja ambayo endapo akitimiza Masharti ya dhamana anapata dhamana na hivyo kurudi nyumbani kwake kuungana na familia yake.
Hata hivyo hadi sasa bado hajatekeleza Masharti ya dhamana bado yupo chini ya Ulinzi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Pole Msoffe na hongera kwakufutiwa Kesi hiyo Ndio Sheria lazima ifuatwe na wale waliopewa jukumu la kusimamia na kutekeleza Sheria.Na Imani kwa kupitia tuhuma zile za Kesi za Mauji na kukusababishia ukaishi gerezani ni wazi utakuwa umejifunza sasa Kuwa Sheria zipo ,hazibagui masikini wala Tajiri wala Mtu maarufu,na dola inanguvu sana kuliko mwananchi wa aina yoyote yule na inamkono mrefu .
Ushauri wangu jiepushe kukaribia au Kutenda mambo yanayovunja Sheria. Msoffe ambaye wewe ni shabiki mwenzangu wa Bendi ya FM academia nakushauri kaa mbali na tuhuma mbaya ambazo umekuwa ukisifika nazo sina haja ya kuzitaja hapa. Nakumbuka Uliwahi kushitakiwa kwa Kesi Moja katika Mahakama ya Kisutu ukaenda Jela kwa kukosa dhamana na Kesi ile ikaisha ila Kesi hii ya Mauji ilisababisha licha na Umaarufu wako wote Ukakaa Jela kwa Kipindi chote hicho.
Nimelazimika kuandika story hii ya Msoffe Kufutiwa Kesi hii Kwani Mimi nilikuwa ni miongoni mwa waandishi wa Habari tuliokuwa siku ya kwanza anafikishwa mahakamani hapo kuandika Habari yake mfululizo hadi baadhi ya ndugu zake wakawa wanatuzuia tusimpige picha na kututolea maneno machafu bila kujua tulikuwa tukitimiza wajibu wetu hadi nilipoacha kazi ya uandishi wa habari katika gazeti la Tanzania Daima Agosti mwaka 2014 ndipo nilipoacha kuandika kesi hii.
Tulishawasamehe.....
Chanzo @Happy Katabazi{Facebook}

No comments:
Post a Comment